Sunday, March 25, 2018

RAIS MAGUFULI AWALILIA 26 WALIOKUFA KWENYE AJALI YA HIACE,LORI PWANI

  Malunde       Sunday, March 25, 2018
Rais Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani kufuatia vifo vya watu 26 ambao wamepoteza maisha katika jali ya basi dogo (Hiace) iliyogongana na Lori katika kijiji cha Mparange Mkuranga mkoani Pwani. 


Rais Magufuli ametuma salamu hizo kwa Mhandisi Evarist Ndikilo na kumtaka amfikishe pole hizo kwa familia za watu ambao wamepoteza maisha katika ajali hiyo mbaya iliyotokea jana tarehe 24 Machi mwaka huu. 

“Nimesikitishwa sana na taarifa ya vifo vya watu 26 waliopoteza maisha katika ajali ya barabarani iliyotokea huko Mkuranga Mkoani Pwani, tumepoteza idadi kubwa ya Watanzania wenzetu na nguvu kazi ya Taifa. Naungana na wafiwa wote katika kipindi hiki kigumu cha huzuni na majonzi ya kuondokewa na wapendwa wao na watu waliowategemea”

Aidha Rais Magufuli amevitaka vyombo vinavyohusika na usalama wa barabarani kuchunguza chanzo cha ajali hiyo na kuchukua hatua zinazostahili lakini pia Magufuli amewaombea marehemu wote wapumzishwe mahali pema na majeruhi 9 wa ajali hiyo wapone haraka ili waungane na familia na jamaa zao kuendelea na shughuli za kila siku.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post