Saturday, March 31, 2018

MPIGA PICHA WA DIAMOND PLATNUMZ 'KIFESI' AACHA KAZI WCB

  Malunde       Saturday, March 31, 2018
Mpiga picha wa msanii Diamond Platnumz na WCB kwa ujumla, Kifesi ameamua kuachana na kazi hiyo.


Kifesi ameeleza kuwa muda aliyofanya kazi WCB wa takribani miaka mitano unatosha ila kilichomsukuma zaidi kuacha kazi ni kutaka kujiajiri na kuwa karibu na Mungu wake kwani kazi aliyokuwa anaifanya ilimbana zaidi. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Kifesi ameandika;


"Leo ikiwa ni siku takatifu na siku ya ibada kwangu ni siku nilioamua kufanya maamzi yatayobadili maisha yangu, nimeamua rasmi kuacha kazi kama mpiga picha wa Diamond na mwajiriwa wa WCB.. 


"Well It’s insane to be leaving a stable job u love But that’s reality for me naacha kazi kwa mtu alikuwa zaidi ya Rafiki kwangu, naacha kazi ambayo ni ndoto ya vijana wengi out there but to me..i see miaka yngu 4/5 ya kufanya kazi hapa inatosha niachie nafasi kwa vijana wengine nimeamua kufata moyo wangu.


"Ni uamzi niliokua nao karibu mwaka sasa but kama ilivyo kwa waajiriwa wengi is so hard kufanya maamzi ya kuacha kazi but IN ORDER TO GROW WE NEED TO MAKE CHANGE.. Naacha kazi to pursue my Dreams life ikiwamo kujiajiri mwenyewe. Naacha kazi ili nipate muda mwingi wa kuwa flexible nitumie muda wangu mwingi ku-unleash my potential for excellence. reason ya mwisho na kubwa zaid kwangu.


"Naacha hii kazi ili niwe karibu zaidi na Mungu wangu kwa imani yangu kama Mkristo nilikua nafanya kazi katika lifestyle na mazingira ya kazi yasiyompendeza Mungu, ilinibidi kujihusisha na mziki, kwenda kwenye matamsha ya mziki, kwenda maeneo ya starehe kutokua na muda wa kwenda kanisani sababu ya kazi at the end we need to choose GOD over everything, sifa, umaarufu na fahari yote ya Dunia vitanifaidia nini endapo nitaukosa ufalme wa Mungu.


"Nimeamaua ku-drop kila kitu i just want to be happy, do my works live my life and have time with God, ukimchagua Mungu hata hivi vingine atakuongezea najua kutakua na changamoto nyingi, Up and downs but Mungu He knew me before was born aliahidi ukimchagua yeye he will open the doors atatufnya kuwa kichwa na siyo mkia.


"Mwisho nashukuru familia yote ya WCB kwa kuwa na mimi for all these years was great working with u.. but zaidi nimshukuru Diamond kwa muda wote niliofanya nae kazi since chini mpaka sasa, nimefnya kazi kwa mapenzi, bidii na uaminifu mkubwa kwangu haukua boss bali rafik na nilkua rafiki wa kweli kwako a will always appreciate mchango wako kwangu.. Tusameheane pale tulipowahi kukoseana we are just humans, hatutakuwa pamoja kikazi but nina imani tutaendelea kuwa marafiki. God bless you, uzidi kufika unapopenda kufika, GOD Bless me.. God bless my next Hustles #happysabbathDay


Utakumbuka Siku chache zilizopita, March 28, 2018 mara baada ya aliyekuwa Baby Mama wa Diamond Platnumz, Zari The Boss Lady kupata dili la kuwa balozi wa bidhaa za Softcare Diapers, Kifesi alitupa lawama kwa Diamond kwa kumuacha Zari kwa kudai alikuwa ni mwanamke wa Baraka aliyepewa na Mungu.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post