MBOWE NA WENZAKE WAFIKISHWA MAHAKAMANI...ULINZI MKALI UMEIMARISHWA ENEO LA MAHAKAMA


Ulinzi  mkali umewekwa leo katika mahakama ya Kisutu jijini Dar es salaam wakati viongozi wa juu wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema ) akiwemo mwenyekiti wa Chama hicho Taifa na kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni Freeman Mbowe akiwa na wenzake.

Mbowe na wenzake wamefikishwa mahakamani hapo chini ya ulinzi mkali Majira ya saa moja asubuhi kwa kwenda kuendelea na kesi inayowakabili na leo kujulikana hatma ya dhamana yao pia.

Wengine waliofikishwa no mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho (Zanzibar) Salum Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho (Bara) na Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Katibu Mkuu wa Chama hicho Vicent Mashinji na wengine.

Na Neema John ,matukiodaimaBlog
Theme images by rion819. Powered by Blogger.