Tuesday, March 20, 2018

MAWAZIRI WAWILI MATATANI...WAMKWAZA RAIS MAGUFULI

  Malunde       Tuesday, March 20, 2018
Waziri wa Kilimo, Dk Charles Tizeba na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina pamoja na Makatibu wao wameshindwa kuhudhuria mkutano wa 11 wa baraza la taifa la Biashara uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam na kuendeshwa na Rais Dkt Magufuli.


Katika mkutano huo Rais Magufuli aliwahitaji mawaziri hao ili waweze kutoa ufafanuzi kuhusu masuala ambayo yameibuliwa na wafanyabiashara, lakini mawaziri hao pamoja na Makatibu wao hawakufika licha ya kuwa walialikwa na kupaswa kuwepo kwenye mkutano huo.


Kufuatia kutokuwepo kwa viongozi hao, Rais Magufuli alimuuliza Waziri Mkuu (Kassim Majaliwa) kama waliweza kuwaalika mawaziri hao na ndipo Waziri Mkuu alipojibu kuwa walipata mualiko na walipaswa kuwepo kwenye mkutano huo ingawa hakukuwa na taarifa yoyote ya wao kutokuwepo wala kutuma wawakilishi wao.


"Kwa hiyo wa Kilimo na Mifugo mawaziri na Makatibu wakuu wote hawapo?............Wao sio wajumbe wa mkutano huu? Alihoji Rais Magufuli ndipo Mawaziri Mkuu aliibuka na kutoa majibu kwa Rais Magufuli.


"Mawaziri wote wanaoguswa na sekta za uwekezaji na "kusupport" uchumi wetu wa viwanda, kilimo ni "facilitater" (msimamizi) wa viwanda na Mifugo naye pia ni wa viwanda walikuwa wapaswa kuwepo hapa kwa sababu walishapewa taarifa wote"
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post