Friday, March 30, 2018

Makubwa Haya : KUTANA NA MWANAMKE ALIYEJIFUNGUA MAPACHA WAWILI WENYE BABA TOFAUTI

  Malunde       Friday, March 30, 2018

Katika hali ya kushangaza huko nchini Uganda, wanaume wawili na watu wengine wamejikuta kwenye mshangao baada ya kukuta wote wawili ni baba wazazi wa watoto wawili mapacha.


Inaelezwa kuwa wanaume hao waliingia kwenye mgogoro siku za hivi karibuni kila mtu aking’ang’ania kuwa baba mzazi wa mapacha hao, na ndipo walipoamua kwenda hospitali ili kupima kipimo cha DNA.

Hata hivyo matokeo ya daktari yalionesha kuwa wanaume hao wote wawili ni baba halali wa mtoto mmoja wa mapacha hao, yaani kila mmoja ana mtoto mmoja kati ya mapacha hao.

Inaeelezwa kuwa wanaume hao Joseph Baseka Sengendo, 25, na Patrick Ssegane, 30, wamezaa na Rashida Nakabugo, ambapo Sengendo anatajwa kuwa mume wa ndoa wa mwanamke huyo.

Wanaume hao wanasemekana kuwa ni ndugu.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post