KIJANA AKAMATWA KWA KUMCHOMA MOTO BABA YAKE MZAZI


Jeshi la Polisi huko Bomet nchini Kenya, linamshikilia kijana mmoja kwa tuhuma za kumchoma moto baba yake mzazi.

Polisi wa eneo hilo wamesema mzee huyo alikwenda kwenye duka la familia ambako mtoto wake huyo yupo na kula vitafunwa, na alipotoka kijana wake alimfuata na kumwagia mafuta ambayo yanaaminiwa ni petroli na kumuwasha moto.

“Baba mtu alipoenda kupata vitafunwa, mmiliki wa duka alimfuata na kumwagia mafuta ambayo tunaamini ni petroli na kumchoma moto”, amesema mkuu wa polisi wa eneo hilo la Bomet, Samson Rukunga.

Mzee huyo aliyechomwa moto amekimbizwa kwenye hospitali ya misheni ya Tenwek ambako anapatiwa matibabu, kutokana na kupata majeraha makubwa ya moto.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.