JESHI LA POLISI LATOA ONYO KWA WANAOTAKA KUANDAMANA

Jeshi la Polisi limetoa onyo kali kwa kikundi kinachohamasisha maandamano ya kuiangusha Serikali kupitia mtandao wa Telegram ambapo limesema kuwa kitendo hicho ni sawa na uhaini.

Akizungumza na vyombo vya habari leo Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa jeshi hilo, Nsato Marijani amesema kwamba kumekuwa na kikundi ambacho kinatumia mtandao huo kuhamasisha maandamano kinyume cha sheria na kutaka kwenda hadi Ikulu kufanya watakayo.

"Sisi kama jeshi la polisi tunawataka kufanya mambo kwa mujibu wa sheria na siyo vinginevyo kwani kitendo cha kufanya maandamano ukiwa na nia ya kuiondoa serikali ni Uhaini. Hatua kali zitachukuliwadhidi ya watu watakaovunja sheria na tusije kulaumiwa kwa lolote," Kamanda Nsato.

Hata hivyo amesema kuwa anaamini wengi wanaopanga mipango hiyo ni vijana na anaamini kuwa wengi wao wameingia huko kwa kufuata mkumbo na kutaka wazazi wachukue nafasi zao kuwaonya watoto wao.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.