DIAMOND AMJIBU TENA SHONZA..."“UNALIJUA LEO BAADA YA KUKOSA POINT SAHIHI?”

Baada ya Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Juliana Shonza kukataa kumjibu Diamond, msanii huyo ameibuka tena yakiwa ni masaa takribani 23 yamepita tangu alipomjia juu kupitia kipindi cha The Playlist.


Diamond ameonekana kukerwa na majibu ya Naibu Waziri Shonza ambayo amekuwa akiyatoa kuhusu kufungia nyimbo za wasanii bila ya kuwapa taarifa sahihi na kuamua kumjibu kwa mara nyingine na safari hii ametumia mtandao wa Twitter.


Kupitia mtandao wa huo Diamond ameandika:
Swala la Barua Unalijua leo baada ya Kukosa Point sahihi? Ungekuwa unajua kama taratibu sahihi ni Kuandika Barua, Mbona hukuwatumia pia Wasanii barua zakuwa unafungia kazi zao?… kwakuwa Uliyapeleka Social Media na Radio, nami nikakupelekea huko ili uenjoy Zaidi…❤



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527