Tuesday, March 20, 2018

MKURUGENZI WA TBC APATA AJALI YA GARI KIGOMA, WATU WAWILI WAFARIKI

  Malunde       Tuesday, March 20, 2018


Na Rhoda Ezekiel- Malunde1 blog

Mkurugenzi wa Shirika la utangazaji TBC Dr. Ayoub Rioba amepata ajali ya gari katika kijiji cha Mgombe kata ya Nyakitonto wilayani Kasulu Mkoani Kigoma wakitokea wilayani Kibondo kuelekea mjini Kigoma.


Akizungumza leo Jumanne Machi 20,2018  mara baada ya tukio hilo kamanda wa Jeshi la polisi  mkoa wa Kigoma Martine Otieno amesema ajali hiyo pia imesababisha vifo vya watu wawili.

  Aliwataja waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni watembea kwa miguu wawili waliofahamika kwa majina ya Teresia Mpoma (55) mkulima na Mkazi wa Nyakitonto na  Yuster Masharubu (55) mkazi wa Nyakitonto.

Ajali hiyo pia imesababisha  majeruhi mmoja aliyefahamika kwa jina la Diana Shedrack (10) mwanafunzi shule ya Msingi Nyakitonto ambaye hali yake ni mbaya na anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Kasulu.


Alisema katika ajali hiyo waliokuwemo kwenye gari ni Mkurugenzi wa Vipindi TBC  Dr. Ayoub Rioba na Meneja wa vipindi kanda ya Magharibi Zabron Mafuru na dereva aliyefahamika kwa jina laAbubakari ambapo wao wamepata majeraha madogo madogo na wamepatiwa matibabu na wanaemdelea vizuri.

Kamanda Otieno alisema chanzo cha ajari hiyo ni utelezi unaotokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika mkoa huo na kuwaomba madereva kuendesha magari kwa umakini kutokana na ubovu wa barabara hiyo na kuzingatia sheria za barabarani.
Muonekano wa gari baada ya ajali hiyo
Kushoto ni Dr. Ayoub Rioba
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post