Saturday, March 31, 2018

BAVICHA KULA PASAKA SEGEREA NA VIGOGO WA CHADEMA WALIOPO GEREZANI

  Malunde       Saturday, March 31, 2018
Viongozi wa Baraza la Vijana Chadema (Bavicha) kesho watasherehekea Sikukuu ya Pasaka kwa kuwatembelea viongozi wa chama hicho waliopo magerezani.Mwenyekiti wa Bavicha, Patrick Ole Sosopi ataongoza msafara wa viongozi wa baraza hilo watakaokwenda Segerea kumtembelea Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe na wenzake.


Amesema wamefikia uamuzi huo kwa lengo la kwenda kuwatia moyo na kuwa nao pamoja.


Amesema viongozi wengine watakwenda Mbeya kwa ajili ya Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi na Katibu wa Chadema, Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga.


"Tunataka kusherehekea nao Pasaka na kuwafahamisha kuwa chama kinaendelea, hatuwezi kurudishwa nyuma wala kutetereshwa,"amesema.


Ole Sosopi pia amewataka vijana wa baraza hilo kuwa tayari kupambana kwa ajili ya chama.


Amesema; "Kuna mambo mengi yanaendelea na tunafahamu wazi kuna ajenda ya kutaka kukifuta Chadema, sasa nawaambia hakuna namna chama hiki kitafutwa, tupo imara na tunazidi kuimarika,'


“Vijana kazi yetu ni kulinda chama na kazi hiyo tutaifanya kwa nguvu zote bila woga, hatutaogopa kufa," amesema.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post