SOSOPI : HILA ZA KUIFUTA CHADEMA HAZITAFANIKIWA....NA HAKUNA WA KUIFUTA CHADEMA

Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la CHADEMA, (Bavicha) Patric Ole Sosopi, amesema kuna lengo la kukifuta Chama hicho kwani nguvu inayotumika kuumiza upinzani hususani CHADEMA ni kubwa sana.

Katika mkutano na wanahabari uliofanyika katika ofisi za chama hicho leo , Sosopi amesema, wapo watu wanaotumwa kuichafua CHADEMA na kupata sababu ya kukifuta chama hicho.

“Tumewapuuza kwa muda mrefu, tukiamini vyombo husika vitachukua hatua dhidi yake lakini kwa kuwa wanamtuma anaendelea kuwa salama. Hila za kuifuta CHADEMA hazitafanikiwa. Kama tulianza na madiwani 3 leo kina zaidi ya madiwani 70 hakitaweza kufutwa kwa njia yoyote" Sosopi.

Amesema Chadema inawahakikishia Watanzania kuwa jitihada za kuifuta CHADEMA hazitafanikiwa na hakuna mtu atakayeifuta CHADEMA.

Sosopi amesema vijana wa CHADEMA wapo tayari kulaumiwa baadaye lakini siyo kuacha chama hicho kiweze kufutwa na kusisitiza kwamba vijana wa chama hicho wako imara na hawaogopi kufa.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.