BAADA YA KUIKUBALI NGOMA YA 'DUME SURUALI'....RAIS MAGUFULI AMEUTAJA WIMBO MWINGINE UNAOMPA RAHALicha ya kuwa na majukumu mengi kama Rais wa nchi na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli lakini ni mtu ambaye anapenda sanaa ikiwa pamoja na kupiga ngoma hata kusikiliza miziki mbalimbali. 

Rais Magufuli mara kadhaaa ameshawahi kutoa sifa kwa baadhi ya wasanii wa bongo fleva na kuwaeleza kufurahishwa na kazi zao, mwaka jana alishawahi kuwasiliana na rapa Mwana FA na kumpa pongezi kwa wimbo wake wa 'Dume Suruali' ambao ameshirikiana na Vanessa Mdee.

Aidha Rais Magufuli pia ameshawahi mweleza msanii Mrisho Mpoto pamoja na Peter Msechu kuwa anavutiwa sana na kazi zao za sanaaa, lakini jana Machi 16, 2018 Rais Magufuli alimweleza rapa Afande Sele ambaye amehamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa huwa anapenda sana wimbo wake wa 'Darubini kali' ambao aliufanya akiwa Morogoro zaidi ya miaka nane iliyopita.

"Nampongeza sana ndugu Selemani Msindi mimi napenda sana nyimbo zake hasa ule wimbo wa Morogoro ninaupenda kweli, amesimama barabarani anafanya hivi anakuwa anapiga miguu hivi kwenda juu kurudi chini polepole, hivyo mimi nampongeza kuamua kurudi CCM" alisema Rais Magufuli.
Chanzo - EATV 
Theme images by rion819. Powered by Blogger.