AMUUA MAMA YAKE MZAZI KWA KUMKATA PANGA BAADA YA KUAMBIWA ANAMROGA


Kijana mmoja aitwae Shazili Saidi Mkuchi mkazi wa Mtwara mwenye umri wa miaka 26, anatafutwa na polisi kwa tuhuma za kumuua mama yake mzazi Bi. Amina Chuwalila kwa kumkata na panga.

Akiongea na mwandishi wa habari kaka wa mtuhumiwa ambaye pia ni mtoto mkubwa wa marehemu anayejulikana kwa jina la Rashidi Saidi Mkuchi, amesema mdogo wake huyo amefanya tukio hilo baada ya kuambiwa na mganga wa kienyeji kuwa mama yake na kaka yake ndiye anayemroga, na kuamua kumfuata shambani alikokuwa na kumfanyia tukio hilo, ambalo limekatisha uhai wake.

“Kama angemkosa mama, basi kifo hiki kingekuwa cha kwangu maana na mimi nimetajwa kuwa nilikuwa nashirikiana na mama yetu kumroga yeye”, amesema kaka wa mtuhumiwa Saidi.

Daktari wa kituo cha afya cha Nanguruwe aliyejulikana kwa jina la Dokta Adam amekiri kumpokea mama huyo akiwa amejeruhiwa vibaya, na kwamba tayari alikuwa ameshafariki.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mtwara Lucas Mkondya amethibitisha kuripotiwa kwa tukio hilo ambalo limetokea Machi 14, na kuwataka wananchi kusaidia kufanikisha kumpata mtuhumiwa huyo ambaye ametokomea kusikojulikana.

Marehem alipokelewa na Dokta Adam wa Kituo cha Afya Nanguruwe na kuthibitisha kuwa alifika Kituoni hapo akiwa tayari Ameshaaga Dunia.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527