Tuesday, March 27, 2018

ALIYEJIFANYA ASKARI NA KULAWITI KISHA KUWAPIGA PICHA ZA UTUPU WANAWAKE AKAMATWA

  Malunde       Tuesday, March 27, 2018

Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro linawashikilia watu 6 akiwemo Mabula Mabula mkazi wa Mji Mpya kwa tuhuma za kujifanya askari na kuwakamata wanawake nyakati za usiku, kuwapora mali, kuwafanyia vitendo vya kikatili kuwalawiti na kuwapiga picha za utupu.


Hayo yamethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Ulrich Matei na kusema kukamatwa kwa mtuhumiwa Mabula ni kufuatia matukio kadhaa ya aina hiyo yaliyo ripotiwa kutokea katika maeneo tofauti ya mji huo.

Kamanda Mtei amesema baada ya kupata taarifa, jeshi hilo kwa kushirikiana na timu ya wataalam wa makosa ya mitandao pamoja na Kikosi cha kupambana na ujambazi wakafanikisha kupatikana kwake ambaye baada ya mtuhumiwa kuhojiwa alikiri kuhusika matukio hayo na kudai anafanya hivyo kwa lengo la kujipatia fedha.

Kwa upande mwingine, Jeshi hilo linawashikilia watu watatu ambao ni vinara wa matukio ya utapeli pamoja na wizi kwa njia ya mtandao wakiwa na simu 9 pamoja na line 57 za mitandao mbalimbali zinazotumika kufanya utapeli.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post