WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA AJIUZULU

Waziri mkuu nchini Ethiopia Hailemariam Desalegn amejiuzulu .

Imedaiwa kuwa kiongozi huyo aliwasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa chama chake cha Ethiopia People's Democratic front. Hatahivyo haijabainika iwapo chama hicho kimekubali uamuzi wake au la.

Waziri mkuu wa Ethiopia amesema kuwa amejiuzulu ili kusaidia kusuluhisha mzozo wa kisiasa uliopo nchini humo.

Taarifa yake ilisema: Wananchi wapendwa, chama tawala cha Ethiopia Peoples Revolutionary Democratic Front na serikali inataka kupata ufanisi wa mabadiliko yaliowekwa katika wakati ambapo kuna mgogoro na matatizo ya kisiasa nchini, ambapo watu wengi wamepoteza maisha, wengine makao huku mali zao zikiharibiwa na kuna juhudi za kuharibu uwekezaji uliopo.
Chanzo- BBC
Theme images by rion819. Powered by Blogger.