Hatari sana!! HII NDIYO MBINU MPYA INAYOTUMIKA KUFANYA BIASHARA YA NGONO...TAZAMA VIDEO | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, February 15, 2018

Hatari sana!! HII NDIYO MBINU MPYA INAYOTUMIKA KUFANYA BIASHARA YA NGONO...TAZAMA VIDEO

  Malunde       Thursday, February 15, 2018

Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi yameendelea kushika kasi kutokana na tabia mbalimbali hatarishi huku makundi maalumu yakiwemo ya watu wanajidunga dawa za kulevya,watu kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja pamoja na biashara ya ngono 'ukahaba'.


Malunde1 blog imekutana na Barthoromeo Zacharia jijini Mwanza, ambaye ni Mdau na Mshauri wa masuala ya kiafya katika kupunguza madhara ya kiafya kwa jamii yanayotokana na VVU/ HIV,TB na dawa za kulevya ambapo ameelezea namna biashara ya ngono hivi sasa inavyofanyika kwa njia za kisasa na kusababisha maambukizi ya VVU kuendelea kuwepo.

Anasema pamoja na njia ya wafanyabiashara ya ngono kujipanga katika barabara ama kupatikana katika maeneo maalum/maarufu ya kufanyia biashara hiyo,pia kuna njia nyingine inayotumiwa na wafanyabiashara hao,matokeo yake wanaume wanajikuta wanafanya ngono bila kujua kuwa wanaofanya nao ni mahahaba.

"Huwezi kumtambua kwa urahisi mtu anayefanya biashara ya ngono kama hujakutana nae kwenye maeneo wanakofanyia,hivi sasa wanatumia mbinu ya 'Nauli' ,hukaa kwenye barabara,baa na maeneo mengine kisha hujirahisha kwa wanaume,wapo tayari kukufuata popote pale ulipo ukishashiriki nae ngono anakuomba pesa ya nauli,huo ndiyo ujira wake"- 

MSIKILIZE HAPA AKIZUNGUMZA.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post