VIONGOZI MBALIMBALI WAMEANZA KUWASILI MAZISHI YA AKWILINA KILIMANJARO

Viongozi mbalimbali wa Serikali wameanza kuwasili nyumbani kwa wazazi wa aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini kijiji cha Marangu, Kata ya Marangu Kitowo, Olele mkoani Kilimanjaro.


Mwili wa mwanafunzi huyo aliyeagwa jana katika viwanja vya NIT, Mabibo jijini Dar es Salaam umefika kijijini hapa leo Februari 23, 2018 saa 3:30 asubuhi.


Viongozi waliofika mpaka sasa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Leonard Akwilapo, Mkuu wa Chuo Cha NIT, Profesa Zacharia Mganilwa pamoja na viongozi wengine wa wilaya.


Ibada ya misa ya kuombea mwili wa marehemu inatarajiwa kuanza saa 6:00 mchana katika kanisa la Mtakatifu Theresia Parokia ya Olele.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.