Tanzia : MSANII WA NYIMBO ZA ASILI KALANGA AFARIKI DUNIA


Msanii Kalanga enzi za uhai wake

Msanii Kalanga enzi za uhai wake
Msanii Kalanga akiwa na Elias Mnyamwezi
***
Habari za kusikitisha zilizolifikia dawati la Nyimbo za asili la Malunde1 blog ni kwamba Msanii wa nyimbo za asili maarufu kwa jina la Kalanga "Ng'wana Kolagwa" amefariki dunia leo Jumatano Februari 21,2018 majira ya saa 11 alfajiri.

Kalanga amefariki dunia nyumbani kwao katika kijiji cha Chambo - Mwamakumbi Nzega mkoani Tabora kutokana na kile kinachoelezwa kuwa alikuwa anaumwa kwa muda mrefu.

Mazishi yanatarajia kufanyika kesho Alhamis Februari 22,2018 saa nane mchana nyumbani kwao.

Malunde1 blog inawapa pole ndugu,jamaa na marafiki bila kuwasahau mashabiki wa marehemu na wapenzi wote wa nyimbo za asili kutokana na msiba huu.

Mungu ailaze Mahali pema peponi roho ya marehemu Kalanga amina!

ANGALIA HAPA BAADHI YA NYIMBO ZA KALANGA


Theme images by rion819. Powered by Blogger.