MWANAFUNZI AFARIKI KWA KUANGUKIWA UKUTA WA DARASA AKIINGIA KWENYE KIPINDI CHA DINI

Mwanafunzi mmoja wa darasa la sita wa Shule ya Msingi
Kibohehe, iliyoko wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, amefariki dunia na wengine watano kujeruhiwa, baada ya kuangukiwa na ukuta.

Mwanafunzi huyo wa kiume ameangukiwa na ukuta wa chumba cha darasa baada ya mvua kubwa iliyoambatana na upepo kunyesha leo Februari 21,2018 mchana.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamis Issah, amesema mwanafunzi huyo alikuwa akiingia kwenye kipindi cha dini na ndipo alipokutana na ajali hiyo ya ukuta na kupoteza maisha

“Mvua ilinyesha na upepo mkali, jengo moja la darasa likadondoka na kumwangukia mtoto huyo ambaye alikuwa akiingia kwenye kipindi cha dini,”amesema Issah.

Aidha Kamanda amesema, majeruhi wamepelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Hai kwa ajili ya matibabu na kwamba uchunguzi zaidi wa tukio hilo bado unaendelea.

Na Florah Temba, Mwananchi
Theme images by rion819. Powered by Blogger.