MAELFU WAUAGA MWILI AKWILINA DAR, MAZISHI KESHO KILIMANJARO

Mwili wa mwanafunzi aliyepigwa risasi na askari polisi siku ya Ijumaa, Februari 16, Akwilina Akwilini, umeagwa rasmi leo na maelfu ya waombolezaji pamoja na wanafunzi wa chuo cha Usafirishaji, na kisha kuanza safari kuelekea mkoani Kilimanjaro kwa mazishi.


Shughuli ya kuaga mwili huo imefanyika leo mchana  katika viwanja vya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), huku pia baadhi ya viongozi mbali mbali wa serikali na watu maarufu wakihudhuria tukio hilo, lililowaacha mamia na machozi ya kumlilia mpendwa wao.


Miongoni mwa waliohudhuria ibada hiyo ni Waziri wa Elimu Joyce Ndalichako, Kamanda wa Polisi Kanda maalum Dar es salaam Lazaro Mambosasa, Msanii Bill Nas, John Mnyika, Salum Mwalimu na wengineo ambao ilikuwa ngumu kuwatambua kutokana na wingi wa watu.


Baada ya Ibada hiyo mwili wa Akwilina ulichukuliwa na kuingizwa kwenye gari maalum tayari kwa kuanza safari, huku ndugu, jamaa na marafiki wakitumia magari ambayo yalikuwepo uwanjani hapo, nhuku wengine wakitakiwa kulipia elfu 40 kwa ajili ya nauli ya kwenda na kurudi mkoani Kilimanjaro

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527