Thursday, February 22, 2018

DIWANI WA CHADEMA MOROGORO AUAWA KWA KUKATWA MAPANGA

  Malunde       Thursday, February 22, 2018Godfrey Luena enzi za uhai wakeDiwani wa Kata ya Namawala wilayani Kilombero, Godfrey Luena (CHADEMA) ameuawa usiku huu wa Februari 22,2018 kwa kukatwa kwa mapanga na watu wasiojulikana nyumbani kwake.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei amethibitisha kuuawa kwa diwani wa Chadema Kata ya Namwawala, Jimbo la Mlimba.

Hata hivyo kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Matei amesema kwa sasa hawezi kufahamu mauaji hayo yanatokana na nini.

Akizungumza kwa simu Kamanda Matei pia amesema kwa sasa ni mapema mno kuwajua watu waliohusika na mauaji hayo na hivyo amewataka wananchi kuwa wavumilivu wakati polisi wakiendelea na uchunguzi wa mauaji hayo.

"Mauaji yametokea usiku huu na polisi wameshafika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa marehemu, sasa hivi tuko kwenye uchunguzi na tunaomba wananchi watusaidie kutoa taarifa za watu wanaodhani kuwa wanahusika kwenye tukio hili na tutahakikisha tunawapata," amesema Kamanda Matei.

Awali mbunge wa Jimbo la Kilombero, Peter Lijualikali alithibitisha mauaji hayo na kudai kuwa yatakuwa yamepangwa.

Amesema kuwa mauaji hayo yametokea saa moja na nusu usiku wakati diwani huyo akiwa nyumbani kwake.

"Akiwa nyumbani kwake ghafla umeme ulikatika, Lwena alitoka nje na kuzunguka nyuma ya nyumba yake kuangalia kama kulikuwa na hitilafu na ndio ghafla lilitokea kundi la watu na kuanza kumshambulia kwa mapanga, " amesema Lijualikali.

Lijualikali amesema kuwa pamoja na watu hao kumshambulia diwani huyo kwa mapanga hadi kufariki lakini pia familia ya diwani huyo imepigwa mawe wakati wakijaribu kupambana na kundi hilo la watu.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post