Makubwa haya : WANAFUNZI WABOMOA NYUMBA YA MWALIMU WAKIDAI KUCHOSHWA NA VISA VYAKE


Wanafunzi wa kidato cha tano na sita katika Shule ya Sekondari ya Lyamungo iliyopo Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro wamevamia nyumba ya mwalimu wa nidhamu wa shule hiyo, Safari Mwasile na kufanya uharibifu kwa madai ya kuchoshwa na visa vya mwalimu huyo.

Aidha, wanafunzi hao pia wamefanya uharibifu katika mashamba ya migomba ya shule hiyo huku wakimtaka Mkurungenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Hai kumwondoa mwalimu huyo, na endapo hataondolewa hawako tayari kuendelea na masomo.

Mmoja wa wanafunzi hao amedai chanzo cha mgogoro huo ulitokana na uchaguzi wa viongozi wa shule ambapo katika upigaji kura mmoja mwanafunzi aliandika matusi kwenye karatasi ya kura.

“Baada utambuzi wa hati mwanafunzi aliyeandika matusi hati yake ilibainika na mwanafunzi huyo alipewa adhabu kurudishwa ya nyumbani kwa muda wa wiki mbili,” amesema.

Inadaiwa mwanafunzi huyo aligomea adhabu hiyo ya kufukuzwa shule huku wanafunzi wenzake wakigoma kuingia darasani wakidai kwamba mwalimu wa nidhamu ndiye chanzo cha matusi hayo.

Na Safina Sarwatt - Mtanzania Kilimanjaro
Theme images by rion819. Powered by Blogger.