MBUNGE WA CHADEMA JOSHUA NASSARI KORTINI KWA SHAMBULIO..AACHIWA KWA DHAMANA


 Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Arumeru kujibu shtaka la shambulio.

Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Fortunatus Muhalila mbele ya hakimu Jasmine Abdul amedai Desemba 14,2014

Nassari alimshambulia Neeman Ngudu.

Anadaiwa kutenda kosa hilo eneo la Makiba kwa kumpiga mateke Ngudu na kumsababishia maumivu akijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.

Muhalila amedai upelelezi wa shauri hilo haujakamilika na ameiomba Mahakama kupanga siku nyingine ya kutajwa shtaka hilo.

Nassari anayetetewa na wakili Sheki Mfinanga alikana kutenda kosa hilo.

Hakimu Abdul aliahirisha kesi hadi Machi 6,2018 itakapotajwa.

Nassari alidhaminiwa na diwani Gabriel Mwanda wa Kata ya Ambuseri aliyesaini bondi ya Sh5 milioni.

Na Mussa Juma, Mwananchi 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527