YANGA BALAA, YAIBAMIZA AZAM 2-1


Klabu ya Yanga leo imefanikiwa kupata ushindi magoli 2-1 dhidi ya Azam Fc , mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Azam complex leo jioni.

Azam ilikuwa ya kwanza kupata goli kupitia kwa mchezaji wake Shaaban Idd katka dakika ya tatu ya mchezo huo.

Dakika ya 30 Chirwa aliipatia Yanga bao la kusawazisha akiunganisha pasi mzuri aliyoipata kutoka kwa Ibrahim Ajib. 

Gadiel Michael aliipatia Yanga bao la pili na la ushindi katika dakika ya 44.

Matokeo ya mechi nyingine za ligi kuu leo ni

Mbeya City 0-0 Mtibwa sugar

Mwadui Fc 2-2 Njombe mji

Kagera sugar 0-0 Lipuli Fc
Theme images by rion819. Powered by Blogger.