WCB WAMTAMBULISHA MSANII MPYA. ITAZAME VIDEO YAKE YA KWANZA HAPA


Lebo ya muziki ya WCB jana usiku ilitambulisha msanii mwingine ambaye kazi zake zitakuwa zikisimamiwa na lebo hiyo, ambapo mbali na kumtambulisha, msanii huyo aliachia ngoma yake ya kwanza akiwa chini ya WCB.


Msanii huyo ni Mbosso ambapo awali alikuwa mmoja kati ya wasanii wanne waliokuwa wakiunda kundi la Ya Moto Band ambalo limesambaratika.


Kabla ya kujiunga na WCB, Mbosso alikuwa akitumia jina la Marombosso.


Hapa chini ni video yake mpya aliyoiachia jana mara baada ya kutambulishwa.

Theme images by rion819. Powered by Blogger.