WATATU WATUPWA JELA MAISHA KWA KUCHOMA MOTO KANISA BUKOBA





Mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba imewahukumu kifungo cha maisha jela washitakiwa watatu baada ya kuwatia hatiani kwa kuchoma Kanisa la EAGT mwaka 2015.


Hukumu imetolewa leo Jumanne Januari 2,2018 na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Charles Oisso baada ya kuridhika na ushahidi uliowasilishwa na upande wa mashtaka kuwa washtakiwa walitenda makosa ya kula njama na kuchoma kanisa hilo eneo la Omukibeta, Manispaa ya Bukoba.


Waliohukumiwa ni Rashid Athuman, Ngesela Ismail na Ally Hassan ambao walidaiwa kutenda makosa hayo kutokana na chuki dhidi ya dini nyingine jambo ambalo Mahakama imesema lingesababisha uvunjifu wa amani na usalama.


Washtakiwa tayari wako gerezani wakitumikia kifungo cha maisha baada ya kutiwa hatiani katika shauri lingine namba 178 la mwaka 2015 ambalo pia linahusu kuchoma makanisa katika maeneo tofauti mkoani Kagera.

Na Phinias Bashaya, Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527