Picha 12 : BABU SEYA NA WANAE WALIVYOKUTANA USO KWA USO NA RAIS MAGUFULI IKULU

Mzee Nguza Vicking(Babu Seya) akifurahi na watoto wake Papii Nguza (Papii Kocha),Nguza Mbangu pamoja na Francis Nguza walipomtembelea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Dkt.John Pombe Magufuli kwaajili ya kumshukuru Ikulu jijini Dar es Salaam.Januari 2,2018.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mzee Nguza Vicking(Babu Seya)aliyeambatana na familia yake kwaajili ya kumshukuru Mheshimiwa Rais Ikulu Jijini Dar es Salaam.Januari 2,2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mzee Nguza Vicking(Babu Seya)pamoja na familia yake walipomtembelea kwaajili ya kumshukuru Mheshimiwa Rais Ikulu Jijini Dar es Salaam.Januari 2,2018.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameshikana mikono na Mzee Nguza Vicking(Babu Seya)pamoja na familia yake wakiomba dua walipomtembelea kwaajili ya kumshukuru Mheshimiwa Rais Ikulu Jijini Dar es Salaam.Januari 2,2018.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mzee Nguza Vicking(Babu Seya)pamoja na familia yake walipomtembelea kwaajili ya kumshukuru Mheshimiwa Rais Ikulu Jijini Dar es Salaam.Januari 2,2018.
Mzee Nguza Vicking(Babu Seya) akizungumza na wanahabari mara baada ya kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Dkt.John Pombe Magufuli walipomtembelea Ikulu jijini Dar es Salaam.Januari 2,2018.
Papii Nguza (Papii Kocha) akionyesha alama ya mchoro unaosomeka ” JPM “mara baada ya kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Dkt.John Pombe Magufuli walipomtembelea Ikulu jijini Dar es Salaam.Januari 2,2018.
Mzee Nguza Vicking(Babu Seya) akiwa na watoto wake Papii Nguza (Papii Kocha),Francis Nguza pamoja na Nguza Mbangu walipomtembelea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Dkt.John Pombe Magufuli kwaajili ya kumshukuru Ikulu jijini Dar es Salaam.Januari 2,2018.

***
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 02 Januari 2018 amekutana na Mwanamuziki Nguza Viking na watoto wake waliofika Ikulu Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kumshukuru kwa kupatiwa msamaha wa kuachiwa huru kwake Nguza Viking (Babu Seya) na Mwanae Papii Nguza (Papii Kocha) waliokuwa wakitumia adhabu ya kifungo cha maisha jela.

Nguza Viking na Papii Nguza wakiwa na wana familia wengine Nguza Mbangu na Francis Nguza wamezungumza na Mhe. Rais Magufuli ambapo wamemshukuru kwa msamaha alioutoa kwao na kwa wafungwa wengine 61 waliokuwa wamehukumiwa adhabu ya kifo, na wamemuahidi kuwa raia wema na watachapa kazi kwa juhudi na maarifa.

“Yaani sijui nisemaje, hapa nina furaha kubwa sana moyoni mwangu, nilikuwa naomba sana tangu muda mrefu nikutane nae, nimeomba sana sana, hatimaye leo nimefanikiwa na nimemwambia namshukuru sana kwa kutusamehe na sasa nipo tayari kuchapa kazi, Hapa Kazi Tu” amesema Nguza Viking na kuungwa mkono na mwanae Papii Nguza.

Nguza Viking na wanae wamemuombea Mhe. Rais Magufuli na wameiombea nchi, na pia msemaji wa familia hii Nguza Mbangu amesema wanajipanga kuendeleza kazi zao za sanaa.

Kwa upande wake Mhe. Rais Magufuli amewashukuru kwa kuja kumuona na kumshukuru lakini amesema shukrani zimwendee Mwenyezi Mungu ambaye ndiye husamehe.

“Najua mmekuwa mkihangaika kutaka kuniona, nikaona wacha niwasikilize, hata hivyo mshukuruni Mwenyezi Mungu ambaye ndiye hutoa msamaha, sasa nendeni mkachape kazi, na mmtangulize Mungu” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli ametia saini kitabu cha maombolezo na kumpa pole Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Kangi Alphaxard Lugola aliyefiwa na Mkewe Kamishna Msaidizi wa Polisi Mary Lugola.

Kamishna Msaidizi wa Polisi Mary Lugola amefariki dunia jana asubuhi tarehe 01 Januari, 2018 katika hospitali ya Rabinisia iliyopo Jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu na msiba upo Gerezani Railway Club Jijini Dar es Salaam.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasilino ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
02 Januari, 2018

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527