WATU 40 MBARONI KWA MAUAJI YA WATU WAWILI BUNDA

Jeshi la Polisi mkoa wa Mara linawashikilia watu zaidi ya 40, wakazi wa Kijiji cha Mikomariro wilayani Bunda kwa tuhuma za mauaji ya watu wawili sababu ikitajwa kuwa ni mgogoro wa mpaka wa shamba.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Jafari Mohamed amethibitisha kukamatwa kwa watu hao huku akiongeza kuwa Jeshi lake bado linawasaka watu wengine waliohusika na tukio la mauaji ya watu wawili wakazi wa Kijiji cha Remng'orori wilayani Serengeti.


Aidha kamanda Jafari amebainisha kuwa waliokamatwa ni wale walioshiriki yowe iliyosababisha mauaji ya watu wawili kwa kuwakata kwa mapanga kwa sababu ya ugomvi wa mipaka ya mashamba.


Amesema kuwa chanzo cha mgogoro huo ni mpaka wa wilaya za Bunda, Serengeti na Butiama ambao unahusisha eneo la ekari 3,535 ambapo Wegesa Gikene na Nyamhanga Gembo wakazi wa Kijiji cha Remng'orori waliuawa kwa kukatwa na mapanga wakati wakiwa shambani.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527