MWANAMKE AUAWA KISHA KUCHUNWA NGOZI...ANYOFOLEWA VIUNGO VYA MWILI NA WASIOJULIKANA

Mwanamke mmoja mkazi wa kijiji cha Mpande mkoani Songwe amekutwa amekufa kwa kupigwa kitu kizito kichwani huku akiwa amechunwa ngozi na kutolewa baadhi ya viungo vya mwili wake na watu wasiojulikana.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Mratibu Msaidizi wa Jeshi la Polisi mkoani hapo Yusuph Sarungi amesema ni kweli tukio hilo limetokea na wameweza kubahatika kumtambua kwa jina marehemu huyo kuwa ni Luntinala Tunyepa mwenye umri wa miaka ipatayo 75.

Aidha, Sarungi amesema mpaka sasa chanzo cha tukio la kuuawa mwanamke huyo hakijafahamika huku akisema wanaendelea na msako mkali ili kuweza kuwabaini watu hao waliotenda hivyo.

Chanzo - EATV
Theme images by rion819. Powered by Blogger.