Saturday, January 27, 2018

MWANAMKE ATEKWA ,ABAKWA KISHA KUUAWA KWA KUMWAGIWA TINDIKALI

  Malunde       Saturday, January 27, 2018
Binti wa miaka 24 mwenye mtoto mmoja ambaye ni raia wa Kenya, ameuawa kikatili baada ya kutekwa na mume wake ambaye alikuwa na rafiki yake kisha kumwambia rafiki yake huyo ammbake binti huyo na baada ya mateso hayo kwa kushirikiana wakamwagia tindikali.


Lucy Ndungu aliwekewa dawa za kulevya na mumewe na ndipo alipoweza kumteka akiwa na rafiki yake, na baada ya kumbaka na kummwagia tindikali waliutupa mwili wake kando ya barabara.


Familia ya marehemu imeeleza kuwa ilimkuta Lucy anamajeraha ya kuungua kwa 75% ya mwili mzima huku hali yake ikiwa mbaya sana na hivyo akawahishwa katika Hospitali ya Taifa Kenyatta kupatiwa matibabu lakini hata hivyo akiwa kwenye matibabu hayo alifariki dunia.


Inaelezwa sababu ya mume huyo kufanya hivyo ni kwamba, walikuwa kwenye ugomvi na Lucy akaamua kuachana naye na kuondoka nyumba waliokuwa wanaishi pamoja na kukataa kurudiana na mumewe huyo jambo ambalo linadaiwa kumkasirisha mwanaume huyo.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post