Thursday, January 4, 2018

MTOTO WA MIAKA MITATU ACHOMWA MOTO KWA KOSA LA KULAMBA SUKARI

  Malunde       Thursday, January 4, 2018
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Jaffary Mohamed amethibitisha kuwa wanamshikilia Nyandaro Kusoya mkazi wa kijiji cha Nyang'oma kwa tuhuma za kumchoma moto mikono yote mtoto wa kaka yake, Sarah Kaela(03) kwa kosa la kulamba sukari.

Akithibitisha tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara amesema mtuhumiwa huyo Nyandaro Kusoya mwenye umri wa miaka 29 alimchoma moto mtoto huyo wa kaka yake, Sarah Kaela mwenye umri wa miaka mitatu kwa kile kinachodaiwa alifanya kosa la kulamba sukari.

Bibi wa mtoto huyo Nyamata Chihoye amesema mtuhumiwa huyo Nyandaro Kusoya alimfuata mjukuu wake huyo na kuondoka naye kwa lengo la kwenda kuishi naye katika kijiji cha Nyang'oma Musoma vijijini Mkoani Mara na matokeo yake kusikia mjukuu wake amefanyiwa kitendo cha kikatili.

Aidha Kamanda Mohamed amesema wanafanya taratibu za kisheria ili kuhakikisha wanamfikisha mtuhumiwa mahakamani.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post