MBOWE : HUWEZI KUMSHAMBULIA ASKOFU KAKOBE KAMA UNASHAMBULIA MTOTO MDOGO

Mwenyekiti wa CHADEMA na Kiongozi Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe amewataka Watanzania kuwa tayari kukosolewa na viongozi wa dini kwani ndiyo wanaoliombea Taifa liwe na amani katika kipindi chote tangu nchi ilipopata Uhuru.


Mbowe ameyasema hayo jana wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari kuhusu hali ya kisiasa kwa mwaka 2017, ambapo alisema kila mtu ana mapungufu katika utendaji wake wa kazi hivyo kila mmoja awe tayari kupokea ushauri kutoka kwa viongozi wa dini.


“Lakini viongozi wetu wa dini wana haki ya kusema, wana wajibu wa kusema, hawa ni watu wanaolea Taifa hili kiroho, huwezi kumshambulia Kakobe kama unamshambulia mtoto mdogo, hawa wana waumini wana followers (wafuasi) na hawa ndiyo kila siku Rais anasema wamwombee, sasa wanamwombea vipi wakati unawapa masharti?,” alisema Mbowe na kuongeza.


“Sisi wapinzani tunakosolewa, viongozi tuwe na unyenyekevu wa kukubali mawazo tofauti tukisemwa, tusijenge chuki katika jamii, vyama vyetu vyote vinaongozwa na binadamu vinaweza vikakosea, tuwaache viongozi wa dini wafanye kazi yao, tukikosea waseme.”

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527