Friday, January 5, 2018

KITABU CHA KASHFA ZA DONALD TRUMP 'FIRE AND FURY' CHAINGIA SOKONI

  Malunde       Friday, January 5, 2018
Mchapishaji wa kitabu chenye utata kuhusiana na rais Donald Trump amesema kuwa amevikabili vikwazo kutoka kwa wanasheria wa Trump wanaojaribu kuzuia kisichapishwe.

Aidha, ametangaza kwamba amechukua hatua kichapishwe mapema, leo Ijumaa na tayari kimeanza kuuzwa katika mtandao wa Amazon.

Bw Trump amesema kwamba kitabu hicho kimejaa "uongo mtupu).

Kitabu hicho awali kilikuwa kimetarajiwa kuchapishwa Jumanne wiki ijayo.

Kitabu hicho kijulikanacho kwa jina la Fire and Fury kilichoandikwa na Michael Wolff kutokana na upinzani mkali wa uchapishwaji wake kwa sasa kinatolewa siku nne kabla ya muda uliotarajiwa.

Mwandishi wa kitabu hicho amethibitisha kupitia ukurasa wake wa Twitter kwamba kitabu hicho kitakuwa sokoni leo.

"Kwa sasa mambo tayari, mtakisoma kesho. Asante sana Trump," amesema mwandishi huyo wa kitabu.

Maoni ya mambo yanayomhusu rais Trump na familia yake yaliyozungumzwa ndani ya kitabu hicho, yametolewa na aliyekuwa msaidizi wa Trump Steve Bannon, zikiwemo tuhuma familia ya Trump kukutana na watu kutoka Urusi ili kuingilia masuala ya uchaguzi wa mwaka jana.
Chanzo- BBC
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post