Friday, December 15, 2017

WATANO WAPANDISHWA KIZIMBANI KWA WIZI WA KUTUMIA MAPANGA

  Malunde       Friday, December 15, 2017

VIJANA wanne na mtoto mmoja wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni kwa wizi wa kutumia mapanga na kuiba fedha na vitu vyenye jumla ya thamani ya Sh milioni 3.35 Washitakiwa waliotenda kosa hilo ni Dimas Denis (20), mkazi wa Kijitonyama, Juma Selemani (22) anafanya kazi ya ulinzi mkazi wa Tandale Tanesco, Karimu Hamisi (23), mkazi wa Ali Maua na mtoto wa miaka 17.

Wakisomewa mashitaka hayo mbele ya Hakimu Hanifa Mwingira, msoma mashitaka Credo Rugaju alidai kwamba washitakiwa hao walitenda kosa hilo Novemba 11 mwaka huu maeneo ya Ali Maua B, wilaya ya Kiondoni jijini Dar es Salaam.

Alidai kwamba watuhumiwa hao waliiba, runinga flat Screen aina ya Boss yenye thamani ya Sh 750,000, kompyuta mpakato aina ya Dell yenye thamani ya Sh 800,000, simu aina ya Iphone Six Plus yenye thamani ya Sh milioni 1.6 na fedha Sh 200,000 vikiwa ni mali ya Cresence Nguzo.

Rugaju alidai kwamba washitakiwa hao baada na wakati wakimuibia Nguzo walimtishia kwa mapanga na kumuibia vitu hivyo. Washitakiwa wote wamekana shitaka hilo, wamerudishwa rumande kwa kuwa makosa kama hayo kisheria hayana dhamana. Washitakiwa hao wanatarajiwa kurudishwa tena mahakamani hapo Desemba 27 mwaka huu, ili kutajwa kesi hiyo.

IMEANDIKWA NA MOHAMED MUSSA- HABARILEO
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post