TANI 11 ZA SAMAKI ZAKAMATWA JIJINI MWANZA

Naibu Waziri wa Uvuvi, Abdalla Ulega, leo Ijumaa amefanya ziara ya kushtukiza katika soko la kimataifa la samaki la Kirumba jijini Mwanza na kukamata tani 11 za samaki waliokuwa wakiandaliwa kusafirishwa nje ya nchi kinyume cha sheria.

Shehena hiyo ya samaki ambao hawaruhusiwi kuvuliwa kisheria, wanadaiwa kuwa walitaka kusafirishwa kwenda nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC) kupitia mpaka wa Rusumo mkoani Kagera.

Pamoja na kukamata samaki hao, naibu waziri huyo pia ameagiza kuondolewa mara moja kutoka sokoni hapo maofisa uvuvi kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela waliokuwa na dhamana ya kusimamia ukaguzi katika soko hilo kwa kushindwa kutimiza wajibu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527