SHIRIKA LA FOUNDATION FOR TOMORROW LATOA TUZO MAALUMU KWA WALIMU BORA MKOA WA ARUSHA


Kushoto aliyevalia koti jeusi ni Mgeni rasmi Mariam Kimoso
ambaye alimuakilisha mkurugenzi wa jiji la Arusha akimkabidhi mwalimu aliyefanya vizuri hivi karibuni katika kinyang’anyiro cha kuwasaka walimu bora lililoendeshwa na shirika lisilokuwa la kiserikali la Foundation For Tomorrow jijini Arusha,katikati ni diwani wa kata ya Themi jijini Arusha,Milance Kinabo, (CHADEMA) .Habari Picha na Pamela Mollel-Arusha
Mkurugenzi wa shirika la Foundation for Tomorrow Melissa Queyquep, akizungumza katika hafla hiyo ambapo alisema kuwa
lengo ni kuwawezesha walimu kupata mamlaka ambayo itawasaidia katika ufundishaji wa wanafunzi bila ubaguzi wowote katika kufufua maendelea ya elimu
Mgeni rasmi Mariam Kimoso ambaye alimuakilisha mkurugenzi wa jiji la Arusha akizungumza katika hafla hiyo
Walimu wakifuatilia hafla hiyo
Mjumbe wa bodi wa shirika la Foundation for Donacian Lyaruu
akizungumza katika hafla hiyo
Diwani wa kata ya Themi jijini Arusha,Milance Kinabo, (CHADEMA),akiteta jambo na Bi.Narja Roel 

Mwalimu Pius Edward kutoka shule ya msingi Sing’isi akipokea
zawadi kwa mgeni rasmi

Mkurugenzi wa Upendo Friends Isabella Mwampamba alisema kuwa mwalimu anatakiwa kuheshimika kwa kazi kubwa ambayo wamekuwa wakifanya hivyo ni muhimu sana kuwatia moyo
Mwenyekiti wa wakuu wa shule jiji la Arusha Msendekwa
Reginard akizungumza katika hafla hiyo
Mkurugenzi wa shirika la Foundation for Tomorrow Melissa Queyquep,akimkabidhi zawadi ya T-shirt diwani kata ya Themi jijini Arusha Milance Kinabo
Mkurugenzi wa Upendo Friends Isabella Mwampamba akiteta jambo na Mkurugenzi wa shirika la Foundation for Tomorrow Melissa Queyquep 
Picha ya pamoja
**
Wadau mbalimbali wa elimu wametakiwa kuunga mkono juhudi
zinazofanywa na taasisi ya Foundation for tomorrow katika harakati za kuwapa uwezo walimu pamoja nakuwapa motisha hali ambayo itasaidia wanafunzi kufanya vizuri zaidi wawapo shuleni

Akizungumza hivi karibu katika Tuzo maalumu ya walimu
iliyoandaliwa na shirika lisilokuwa la kiserikali la Foundation For Tomorrow, Mgeni rasmi Mariam Kimoso ambaye alimuakilisha mkurugenzi wa jiji la Arusha,alisema kuwa walimu wanakazi kubwa sana hivyo ni vyema wakapongezwa kwa kazi nzuri wanayofanya.

Alisema  elimu kubwa inayotolewa na walimu kwa wanafunzi
mashuleni itasaidia kuleta mandeleo na jamiii nzima itafaidika kupitia elimu hiyo

Mkurugenzi wa shirika la Foundation for Tomorrow Melissa Queyquep, alisema kuwa lengo ni kuwawezesha walimu kupata mamlaka ambayo itawasaidia katika ufundishaji wa wanafunzi bila ubaguzi wowote katika kufukia maendelea ya elimu

“Mamlaka hayo ni kusimamia mitahala vyema huku walimu ambayo watakaoweza kufanya hivyo kuwapongeza ili wawezekufundisha wanafunzi vyema katika kufikia malengo endelevu kwa wanafunzi”,alisema Melissa.

Aidha alisema kuwa shirika hilo linalenga katika kuwapa
wanafunzi uwezo wa kuchochoea na kuchambua mawazo wawapo mashuleni,kuwasaidia wanafunzi wanaohitahi kujifunza zaidi.

Kwa upande wake mkurugenzi wa Upendo Friends Isabella Mwampamba alisema kuwa mwalimu anatakiwa kuheshimika kwa kazi kubwa ambayo wamekuwa wakifanya hivyo ni
muhimu sana kuwatia moyo. 

Na Pamela Mollel-Arusha

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527