SERIKALI KUFUTA UTITIRI WA MIFUKO YA JAMII TANZANIA

Rais John Magufuli amesema Serikali ina mpango wa kufuta utitiri wa mifuko ya hifadhi ya jamii na kubakiza miwili.


Amesema mifuko itakayobaki ni kwa ajili ya kuhudumia wafanyakazi wa sekta binafsi na ya umma.


Rais Magufuli amesema Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) litabaki kwa ajili ya kuhudumia wafanyakazi wa sekta binafsi wakati mifuko mingine yote itaunganishwa na kuwa mmoja.


Amesema hayo jana Alhamisi Desemba 14,2017 alipofungua mkutano mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) mjini Dodoma.


Mifuko mingine inayotoa huduma ya hifadhi ya jamii ni PSPF, LAPF, PPF na GEPF.


Rais Magufuli alisema baadhi ya mifuko ya hifadhi ya jamii imekuwa haiwasaidii wafanyakazi badala yake imekuwa ikiwekeza kwenye ujenzi wa majengo makubwa.


“Mifuko hii haiwanufaishi wafanyakazi bali wapiga dili ambao huamua majengo yajengwe na wao kupata asilimia 10,” alisema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527