Friday, December 15, 2017

Picha : MAMIA SHINYANGA WAJITOKEZA KUMZIKA ASKARI WA JWTZ ALIYEUAWA KONGO

  Malunde       Friday, December 15, 2017

Mamia ya waombolezaji wakiwemo askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),viongozi wa serikali na vyama vya siasa na wananchi leo Ijumaa Disemba 15,2017 wamejitokeza kumzika askari wa JWTZ Private Saleh Said Mahembano (30) katika makaburi ya nyumbani kwao katika mtaa wa Isaka Station kata ya Isaka halmashauri ya Msalala wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.Private Mahembano ni miongoni wa askari 14 waliouawa nchini Kongo Disemba 8,2017 wakati wakitekeleza jukumu la ulinzi na amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambapo walivamiwa na waasi waliojulikana kuwa ni ADF na kusababisha mauaji kwa wanajeshi 14 na wengine 44 kujeruhiwa.Mazishi ya Private Mahembano aliyezikwa kwa heshima za kijeshi yameongozwa na Kamanda wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kanda ya Shinyanga,Kanali Mussa Kingai.Akizungumza wakati wa mazishi hayo,Kanali Kingai alisema kifo cha Mahembano ni cha kishujaa kwani aliweza kutoa upinzani kwa adui aliyewashambulia.

“Askari hawa waliopoteza maisha ni mashujaa wetu,tunawaenzi sana,inawezekana kwa kitendo walichokifanya historia ya Kongo itabadilika,serikali imetoa maagizo uchunguzi ufanyike kuhusu tukio hili,na kama kuna itabainika kuna mtu alitusaliti hatua zitachukuliwa”,alisema Kanali Kingai.

Kanali Kingai alitumia fursa hiyo kuipa pole familia ya marehemu na wananchi kwa ujumla kufuatia kumpoteza mpendwa wao.

Akitoa salamu za pole,Katibu tawala wilaya ya Kahama,Timoth Ndanya aliyemwakilisha mkuu wa mkoa wa Shinyanga na mkuu wa wilaya ya Kahama aliiomba familia ya marehemu na wananchi kuwa na subira katika kipindi hiki kigumu na kwamba wanajeshi hao 14 waliouawa ni mashujaa wa Tanzania.

Akisoma historia fupi ya marehemu,Meja Josephat Mtaki alisema marehemu alijiunga na JWTZ mwaka 2011,ametumikia jeshi miaka 6,miezi 7 na siku 6,ameacha watoto watatu.


ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI WAKATI WA MAZISHI
Askari wa JWTZ wakiwa wamebeba mwili wa wa askari wa JWTZ Saleh Said Mahembano (30) leo kabla ya mazishi katika mtaa wa Isaka Station kata ya Isaka wilayani Kahama - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog 
Mwili wa askari wa JWTZ Saleh Said Mahembano (30) ukiswaliwa kabla ya mazishi katika makaburi ya nyumbani kwao eneo la Isaka Station kata ya Isaka wilaya ya Kahama leo Ijumaa Disemba 15,2017- Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog 
Askari wa JWTZ wakiwa msibani
Waombolezaji wakiwa katika makaburi ya familia ya marehemu
Mazishi ya askari wa JWTZSaleh Said Mahembano (30) yakiendelea
Askari wa JWTZ wakiwa katika makaburi ya familia ya marehemu Saleh Said Mahembano wakati wa mazishi
Mazishi yanaendelea
Mamia ya waombolezaji wakiwa katika kaburi la Mahembano
Swala wakati wa mazishi
Wananchi na askari wa JWTZ wakifuatilia mazishi hayo
Askari wa JWTZ wakitoa heshima za mwisho kwa marehemu
Taratibu za kijeshi zikiendelea
Askari wa JWTZ wakiwa mbele ya kaburi la Mahembano
Taratibu za kijeshi zikiendelea
Askari wa JWTZ wakitoa heshima zao za mwisho kwa Mahembano
Askari wa JWTZ wakijiandaa kupiga risasi tatu tatu hewani kila mmoja
Askari wa JWTZ wakiendelea na taratibu za kijeshi kwenye kaburi la marehemu Saleh Said Mahembano
Kamanda wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kanda ya Shinyanga,Kanali Mussa Kingai akitoa salamu za pole kwa familia,JWTZ na wananchi kwa ujumla kutokana kifo cha askari Saleh Said Mahembano
Kanali Kingai akizungumza wakati wa mazishi ya askari wa JWTZ Saleh Said Mahembano
Kamanda wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kanda ya Shinyanga,Kanali Mussa Kingai akipeana pole na Katibu tawala wilaya ya Kahama Timoth Ndanya
Kamanda wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kanda ya Shinyanga,Kanali Mussa Kingai akitoa pole kwa viongozi mbalimbali wa JWTZ
Meja Josephat Mtaki akisoma historia fupi ya marehemu Saleh Said Mahembano
Meja Josephat Mtaki akisoma historia fupi ya marehemu
Msemaji wa familia ya marehemu,Sheikh Mohamed Athuman akitoa shukrani kwa watu mbalimbali waliojitokeza katika msiba huo
Mwenyekiti wa wananchi wanaotoka Isaka waishio jijini Dar es salaam, Mtakwa Wilson akitoa salamu za pole kwa familia
Katibu tawala wilaya ya Kahama Timoth Ndanya akitoa salamu za pole kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga na mkuu wa wilaya ya Kahama
Timoth Ndanya akizungumza msibani
Waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu Saleh Said Mahembano
Kamanda wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kanda ya Shinyanga,Kanali Mussa Kingai akiteta jambo na mmoja wa wanafamilia ya marehemu Saleh Said Mahembano baada ya mazishi
Kamanda wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kanda ya Shinyanga,Kanali Mussa Kingai akizungumza jambo na mmoja wa wanafamilia ya marehemu baada ya mazishi
Katibu tawala wilaya ya Kahama,Timoth Ndanya akizungumza jambo wakati wa kikao cha familia ya marehemu Saleh Said Mahembano na viongozi wa JWTZ baada ya mazishi.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post