Friday, December 15, 2017

CCM YAWEKA HADHARANI MAJINA YA WAGOMBEA WATATU WA UBUNGE

  Malunde       Friday, December 15, 2017


 Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) imepitisha majina matatu ya wagombea ubunge watakaopeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mdogo utakaofanyika Januari 13, mwakani.


Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho Humphrey Polepole leo Desemba 15, imewataja waliopitishwa kuwa ni Monko Justine Joseph (Singida Kaskazini), Damas Ndumbaro (Songea Mjini) na Dk Stephen Lemomob Kiruswa (Longido).

Amesema CCM kinawatakia wagombea hao maandalizi mema ya uchaguzi chini ya uongozi wa uratibu wa mkoa, wilaya na majimbo husika.

“ Hii itajumuisha kuchukua fomu za uteuzi kutoka Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC) kuanzia Kesho Disemba 16,” amesema.

Wakati CCM kikitangaza wagombea wake, Chama cha ACT-Wazalendo kinakutana kesho jijini Dar es Salaam kujadili uchaguzi huo huku Chama cha Wananchi (CUF) tayari kikiwa kimepitisha wagombea wake.

Na Ephrahim Bahemu, Mwananchi
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post