JAMAA APIGWA NA KUNDI LA WANAWAKE AKIMTAKA MKEWE APISHE KITANDANI ILI ALALE NA MWANAMKE MWINGINE
Picha haihusiani na habari hapa chini

Kundi la wanawake katika Mtaa Majengo wilayani Kahama mkoani Shinyanga wamemshambulia kwa kumpiga mkazi wa mtaa huo aliyefahamika kwa jina la Andrew baada ya kwenda na mwanamke mwingine nyumbani kwake na kumtaka mke wake awapishe kitandani ili walale.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo ambapo majirani hao walifikia hatua hiyo baada ya kuamshwa na kelele zilizokuwa zikiendelea baina ya wanandoa hao.

Akizungumza na Kahama fm, Mke wa mwanaume huyo, Mariam Abdallah, (32) amesema mume wake alifika usiku majira ya saa tano akiwa na mwanamke huyo ambapo alimtaka awapishe kitandani ili walale na yeye akalale sebuleni.


Hata hivyo baada ya kuona hivyo walianza malumbano ndipo majirani walipofika na kuanza kumshambulia mume wake wakisema amewadharirisha wanawake wa eneo hilo.

Kwa upande wake mume wa Mke huyo bwana Andrew amesema mwanamke huyo ni mke wake wa pili, na kwamba alifika nyumbani kwa lengo la kujiandaa kwenda kumpokea mama yake mzazi aliyekuwa anatoka Dar es Salaam ambapo wangeenda wote watatu kwa kuwa alishawatambulisha.

Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha dawati la jinsia na watoto kutoka jeshi la Polisi wilayani Kahama, Gumba Mipawa amethibitisha kutokea tukiko hilo na kwamba wanaendelea kuwahoji wanandoa hao.

Kwa mujibu wa kitengo cha dawati la jinsia wilayani humo, hilo ni tukio la kwanza kuripotiwa kwenye kitengo hicho tangu kianzishwe wilayani humo.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.