Thursday, December 14, 2017

Makubwa Haya!! KIJANA AJICHARANGA VIWEMBE KICHWANI BAADA YA KUACHISHWA KAZI YA KUOSHA MAGARI KAHAMA

  Malunde       Thursday, December 14, 2017
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Kijana Mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Adam (18) amejichana chana na wembe sehemu za kichwani hali iliyosababisha atokwe damu nyingi kwa kile kinachodaiwa kuwa ameachishwa kazi ya kuosha mabasi ya Kampuni ya Rungwe mjini Kahama mkoani Shinyanga.


Tukio hilo limetokea leo Alhamis Disemba 14,2017 majira ya saa tatu asubuhi, baada ya kijana huyo kwenda kwa mwajiri wake kudai arejeshwe kazini lakini alikataliwa na kudaiwa kuanza kufanya fujo na kisha kufikishwa kituo cha polisi Kahama.


Mmoja wa Mashuhuda amezungumzia tukio hilo na kudai kuwa imetokea baada ya kijana huyo kuwa amelewa sana.


Naye wakala wa mabasi ya Rungwe John  Lucas ambapo kijana huyo alikuwa anafanya kazi amesema kijana huyo aliachishwa kazi ya kuosha mabasi ya kampuni hiyo zaidi ya wiki mbili na kwamba leo alifikia hapo saa 12 asubihi kuomba arejeshwe kazini huku akitumia nguvu kudai maombi hayo.

Hata hivyo wananchi kwa kushirikiana na jeshi la Polisi wamempeleka katika hospitali ya mji wa Kahama kwa ajili ya kupatiwa huduma ya matibabu.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post