Sunday, December 17, 2017

MSICHANA ALIYEBAKWA NA WALIMU WAWILI KWA WIKI TATU HOI HOSPITALI

  Malunde       Sunday, December 17, 2017

Msichana wa India ambaye alidaiwa kubakwa na walimu wawili wa shule katika kipindi cha wiki tatu yuko katika hali mahututi baada ya kulazimishwa kutoa mimba.

Madaktari wameiambia BBC idhaa ya Hindi kuwa ubongo wake umeharibika.

Polisi imemtia nguvuni Mkuu wa shule yake na mwalimu wake katika jimbo la kaskazini mwa India la Rajasthan.

Polisi wanasema kuwa alipoteza fahamu baada ya washukiwa kumlazimisha kutoa mimba katika hospitali ya kibinafsi.

Polisi pia wanachunguza nafasi ya hospitali katika tukio hilo.

Msichana huyo mwenye umri wa miaka 18 alilazwa hospitalini baada ya kuhisi maumivu makali ya tumbo na wahudumu katika shule yake wakabaini kwamba alikuwa mjamzito.

Hali yake ya afya ilianza kuwa mbaya kwa haraka baada ya kuavia mimba, lakini haijafahamika wazi ni nini hasa kilichoifanya hali yake kuwa mbaya,alisema polisi katika wilaya ya Sikar said.

Shule hiyo iliyopo wilaya ya Sikar, imefungwa kwa sasa na mamlaka katika eneo hilo.

Polisi wanaamini kuwa masomo ya ziada yanayotolewa katika saa ambazo si za kawaida yalitumiwa kuwaita wanafunzi ili kuwezesha vitendo kama hivyo vya unyanyasaji kufanyika.

Bado polisi hawajaweza kurekodi taarifa kutoka kwa muathirika.

"Hili ni tatizo baya na hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wahusika ,"alisema afisa wa polisi Kushal Singh.
Chanzo- BBC
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post