MAAFISA FEKI WA TAKUKURU WANASWA WAKIPOKEA RUSHWA IKULU


Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa TAKUKURU  mkoani Katavi imewakamata Nicodemo Peter na Peter Mwaninsawa wakazi wa Mtaa wa Nsemlwa Manispaa ya Mpanda kwa tuhuma za kupokea rushwa ya Tshs 400,000 wakati wakiwa nje ya jengo la Ikulu ndogo ya Mkoa wa Katavi baada ya kuijifanya wao ni maafisa wa TAKUKURU.

Wahumiwa hao wawili walikamatwa leo Alhamis Disemba 14,2017 majira ya saa nne asubuhi wakiwa wanapokea kiasi hicho cha fedha katika eneo la nje ya jengo la Ikulu ndogo ya Mkoa wa Katavi iliyopo jirani na ofisi ya TAKUKURU.

Kamanda wa Takukuru wa Mkoa wa Katavi John Minyenya aliwaambia wandishi wa Habari ofisini kwake kuwa watuhumiwa hao walikamatwa kufuatia mtego ulioandaliwa na taasisi hiyo baada ya kuwa wamepata taarifa kutoka kwa msiri wao juu ya watu hao waliokuwa wakijiita ni maafisa wa TAKUKURU wa kitengo cha uchunguzi.

Alisema kabla ya kukamatwa kwa wahumiwa hao walimpigia simu msiri wa TAKUKURU na kujitambulisha kuwa wao ni maafisa wa TAKUKURU na wanalo jalada la uchunguzi za huhuma zinazomkabili msiri huyo.

Watuhumiwa hao walimtaka awape kiasi cha shilingi laki nne ili waweze kulifunga jalada kwa kufuta tuhuma zilizomkabili msiri huyo ambae ni Mtendaji wa Kijiji cha Vikonge Wilayani Tanganyika ambaye walidai kuwa alikuwa na tuhuma za kupokea rushwa ya kutoka kwa wafugaji ambao alikamata mifugo ya wafugaji na kisha aliiachia baada ya kupokea rushwa kiasi cha Tshs 2,500,000/= .

Minyenya alieleza kwa kuwa msiri huyo ambaye hapendi na anapinga rushwa alilazimika kufika kwenye ofisi ya Takukuru na kutoa taarifa juu ya maafisa hao bandia wa Takukuru .

Ndipo Takukuru walipoanza kufanya uchunguzi juu ya malalamiko hayo kutokana na TAKUKURU kutokuwa na watu wenye tabia kama hiyo ya kuomba na kupokea Rushwa.

Alisema ndipo hapo TAKUKURU walipoandaa mtego wa kuwakamata watuhumiwa hao ambao walimtaka msiri huyo awapelekee fedha hizo nje ya jengo la Ikulu ndogo ya Katavi kwa kuwa ni jirani na ofisi yao ya Takukuru ili iwe rahisi wao kutoka ndani ya osisi ya TAKUKURU na kufika kwenye eneo la tukio.

Kufuatia makubaliano hayo msiri ulipofika muda wa kupeleka fedha kwa maafisa hao bandia alikwenda kuchukua fedha zilizokuwa na namba za TAKUKURU na kisha aliwapelekea kwenye eneo walilokuwa wamekubaliana kwa ajiri ya kubabidhiana na mara tuu walipo pokea fedha hizo nje ya jengo la Ikulu watuhumiwa hao walikamatwa na Maafisa wa TAKUKURU huku wakiwa na fedha hizo.

Kamanda Minyenya alisema watuhumiwa hao wanaendelea kushikiliwa na watafikishwa mahakamani ili wakaweze kujibu mashita mawili ambayo ni kujifanya maafisa wa TAKUKURU  na shitaka la pili ni kuomba na kupokea rushwa.
Na Walter Mguluchuma – Malunde1 blog Katavi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527