Thursday, December 14, 2017

CHADEMA YAZUNGUMZIA MBUNGE WAO KUTIMKIA CCM

  Malunde       Thursday, December 14, 2017
Barua na video iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ikieleza mbunge wa Siha (Chadema) mkoani Kilimanjaro, Dk Godwin Mollel amejiuzulu ubunge imezua mjadala.


Katibu wa Chadema Mkoa Kilimanjaro, Basil Lema leo Alhamisi Desemba 14,2017 amesema naye ameona video na barua kwenye mitandao ya kijamii lakini hawana uthibitisho wowote.


"Mheshimiwa Mollel hakuwahi kuonyesha dalili yoyote kuwa yuko kwenye hilo wimbi na mimi nimeona hiyo barua na video kwenye mitandao. Bado kwangu nachukulia kama uvumi mpaka tutakapothibitisha," amesema.


Lema amesema kwa utaratibu alipaswa kumuandikia barua Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe au viongozi wa Chadema.


Amesema akiwa katibu wa mkoa wa chama hicho hajapokea barua yoyote kutoka kwa Dk Mollel.


"Ukiangalia hata barua inayosambaa haijasainiwa na video inaonyesha ni mtu tu kajirekodi akarusha. Katika mazingira hayo hatuwezi kukurupuka kuzungumzia hilo jambo," amesema.


Taarifa inayosambaa kwenye mitandao ambayo haina saini inaonyesha kuandikwa na Dk Mollel akieleza ameamua kujivua uanachama wa Chadema kuanzia leo Alhamisi Desemba 14,2017.


Pia, ametangaza kujiuzulu nafasi ya ubunge na kwamba huo ni uamuzi wake alioufanya akiwa na akili timamu na hajashinikizwa na mtu yeyote.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post