CHADEMA WACHEKELEA RAIS MAGUFULI KUMWACHIA HURU BABU SEYA,PAPII KOCHA




Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimempongeza Rais John Magufuli kwa kutekeleza ahadi zilizotolewa na mgombea urais wa chama hicho, Edward Lowassa ikiwemo ya kuwaachia huru wanamuziki Nguza Viking na Johnson Nguza ‘Papii Kocha’.


Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi na chama hicho imeeleza kuwa katika ahadi zake Lowassa aliahidi iwapo Chadema ingeshinda uchaguzi angewaachia wanamuziki hao.


Vilevile chama hicho kimetoa wito kwa Serikali kutumia mamlaka yake kwa mujibu wa sheria kuondoa nia ya kuwashtaki masheikh wa Zanzibar na mahabusu na washtakiwa wa makosa ya mtandao.


Ombi hilo pia limewagusa mahabusu wa makosa ya kisiasa, ikiwemo kesi za uchochezi zinazohusisha kumkosoa Rais, chama na serikali yake.








Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527