BENKI KUU ( BOT ) YAIAGIZA AIRTEL KUPELEKA TAARIFA ZAKE ZA FEDHA TANGU MWAKA 2000

Kufuatia sakata la umiliki wa kampuni ya mawasiliano ya Airtel, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Disemba 28, 2017 iliziandikia benki zote na taasisi za kifedha ambazo zimekuwa zikisimamia akaunti za iliyokuwa Celtel, Zain au Airtel kuwasilisha taarifa hizo.


BoT imezitaka taasisi hizo ama benki kueleza kama zimewahi kuendesha ama zinaendesha akaunti zinazohusiana na kampuni tajwa.


Aidha, taasisi zote ambazo zitakuwa zina akaunti za kampuni hiyo tajwa, zimetakiwa kuwasilisha jina la akaunti, namba ya akaunti, aina ya fedha zilizomo kwenye akaunti na kiwango cha mwisho kilichokuwemo kwenye akaunti hadi Disemba 27, 2017.


Taarifa za akaunti hizo zinazotakiwa kuwasilishwa ni kaunzia Januari 1, 2000 hadi Disemba 27, 2017.


Taarifa zinazotakiwa kuwasilisha zinatakiwa kuwa katika nakala ngumu (hardcopy) na nakala teke (soft copy) na zilitakiwa kuwasilishwa jana saa 5 asubuhi.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527