Matangazo ya Moja kwa Moja : SHEREHE ZA KUAPISHWA UHURU KENYATTA KUWA RAIS WA KENYA


Ni siku nyingine ambayo Taifa la Kenya leo linatekeleza shughuli muhimu ya kikatiba ya kumuapisha kiongozi wa taifa hilo kufuatia ushindi wake wa marudio ya uchaguzi wa Oktoba 26 uliosusiwa na upinzani.


Uhuru Kenyatta leo anaapishwa rasmi kuwa rais wa nchi hiyo kwa muhula wa pili baada ya kuibuka mshindi kwenye uchaguzi mkuu.


Wageni mbalimbali wanatarajiwa kushuhudia sherehe za kuapishwa kwa kiongozi huyo wa Kenya huku ulinzi ukiimarishwa kila kona


Uchaguzi wa uliofanyika Agosti ulifutwa na mahakama kutokana na kile kilichotajwa kuwa uchaguzi usio huru na haki.


Marudio ya uchaguzi wa Oktoba 26 ulimpatia Uhuru Kenyatta asilimia 98 ya kura huku waliojitokeza kushiriki katika shughuli hiyo wakiwa na asilimia 39.


==>Tazama tukio hilo hapo chini

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527