WAKUU WA MIKOA WABANWA KUJENGA VIWANDA VIPYA 100 NDANI YA MIEZI 12


WAZIRI wa Nchi - wala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Suleiman Jafo amewataka wakuu wa mikoa nchini, kuhakikisha kuwa kila mmoja anajenga viwanda vipya 100 kuanzia Desemba 2017 hadi Desemba 2018.


Akizungumza na wakuu wa mikoa wapya walioapishwa juzi Ikulu, na kufanya nao mazungumzo jijini Dar es Salaam, Jafo alisema lengo la Serikali ni Desemba 2018, mikoa yote 26 ya Tanzania Bara inakuwa na viwanda vipya 2,600.

Waziri Jafo alisema Serikali ya Awamu ya nchi ya uchumi wa kipato cha kati kupitia ujenzi wa viwanda, hivyo aliwataka wakuu wa mikoa yote, kuibua viwanda vidogo na vya kati kwa kuhamasisha ushiriki wa viongozi ndani ya mikoa na wananchi wote katika maeneo yao ya utawala.

Aliongeza kuwa katika kusimamia utekelezaji itaweka utaratibu maalumu wa kupima utendaji kazi wa kila kiongozi wa mkoa katika kuangalia ushiriki wake wa kuwajengea hamasa viongozi wa chini wakiwemo wakuu wa wilaya na wananchi.

“Serikali itatoa vyeti kwa mikoa yote itakayofanya vizuri katika ujenzi wa viwanda, hatua hii inalenga kutoa motisha kwa mikoa iliyobaki kuweza kujifunza na kubaini mbinu mbadala katika kuibua viwanda ili kuweza kuwakomboa kiuchumi wananchi,” alisema Jafo.

Kwa mujibu wa Jafo, katika kufanikisha dhana ya ujenzi wa uchumi wa viwanda nchini, serikali inaendelea kuweka mkazo na kipaumbele katika upakilimo, na hivyo kuwataka wakuu wa mikoa kuhakikwanatekeleza vyema majukumu yao ya kazi.

Aidha Jafo aliwataka wakuu wa mikoa, kusimamia vyema makusanyo ya fedha za ndani zinazokusanywa katika halmashauri zote nchini na kutumia vyema fedha za asilimia 5 zilizotengwa katika halmashauri kuwawezesha na kuhamasisha wananchi kupata mikopo ili kuwawezesha kushiriki katika ujenzi wa uchumi wa viwanda.

Aliwataka wakuu wa mikoa kuwaelekeza maonchini kuweza kuhamasisha wananchi kujiunga katika vikundi vya ushirika ili weweze kupatiwa mikopo kupitia mifuko ya fedha inayotolewa na serikali na hivyo kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima alisema ili kufanikisha dhana ya uchumi wa viwanda, serikali haina budi kuwapa msukumo na ushirikiano wa karibu wanasayansi ili kuwawezesha kuibua viwanda vingi zaidi pamoja na kuhakikisha upatikanaji nchini.

Wakati huo huo, Naibu TAMISEMI, Tixon Nzunda aliwakumbusha wakuu wa mikoa kuhakikisha pia wanatenga maeneo kwa ajili ya ujenzi wa viwanda, wahakikishe kuwa wananchi hawavamii maeneo ya shule na pia wafanye maandalizi ya kutosha kuhakikisha kuwa wanafunzi wote waliofaulu darasa la saba wanapata nafasi ya kusoma sekondari.

Mbali na Malima, Wakuu wengine wa Mikoa waliohudhuria mkutano huo ni Robert Luhumbi (Geita), Joachim Wangabo (Rukwa), Galesius Byakanwa (Mtwara) na Christine Mndeme (Ruvuma).

Pia kikao hicho kilihudhuriwa na viongozi TAMISEMI akiwepo Nai- TAMISEMI, Josephat Kandege na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), Ronald Lwakatare.

Chanzo-Habarileo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527