Video: NJIWA MWENYE HIRIZI AZUA GUMZO UNGUJA...ANAZURURA SANA NA HAKAMATIKI


Njiwa akiwa amefungwa Hirizi nyekundu akutwa akitembea katika mazingira tofauti katika kisiwa cha Uzi Mkoa wa Kusini Wilaya ya Kati Unguja.

Baadhi ya Wananchi walioshuhudia tukio hilo wamesema wamethibitisha kuwa tangu tarehe 3 Septemba njiwa huyo alionekana katika mazingira tofauti ikiwemo mtaa wa Nyeke Mikokoni .

Wamesema wametafuta njama mbadala za kutaka kumkamata njiwa huyo lakini hawakufanikiwa kumtia mikononi.

Wakazi wa Kijiji hicho cha Uzi wameshangazwa sana na tukio hilo kwani hawafahamu mtugani aliempachika hirizi njiwa huyo na pia lengo gani lililopelekea hata njiwa huyo akavishwa kifaa hicho.

Video ikimuonesha njiwa mwenye hirizi akipuyanga.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post