Tanzia : MBUNGE WA CUF AFARIKI DUNIA

Mbunge Mteuliwa wa Viti Maalum wa Chama cha Wananchi (CUF), Bi. Hindu Hamis Mwenda amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa CUF, Abdul Kambayaimeeleza kuwa Bi. Hindu alifariki dunia jana jioni akiwa Muhimbili alipokuwa akitibiwa baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Kiongozi huyo hakuweka wazi kuwa Mbunge huyo mteule alikuwa akisumbuliwa na tatizo gani, lakini alisema taratibu nyingine za mazishi zitatolewa.

Bi Hindu alikuwa miongoni mwa wabunge 8 wapya wa CUF walioteuliwa na chama hicho kujaza nafasi zilizoachwa wazi na wabunge waliofutwa uanachama.

Uteuzi huo ulitangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Julai 27 mwaka huu na wabunge hao nane walikuwa wanatarajia kuapishwa juma lijalo wakati wa kuanza kwa vikao vya bunge mjini Dodoma.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post